Jihusishe

Jiunge na zaidi ya wenyeji 60,000 ambao hutoa makazi ya dharura wakati wa shida.
Mwanamke anatandika kitanda katika chumba safi cha kulala chenye mwanga wa jua, kitanda chenye mihimili minne na kasha la mbao kwenye tendegu.

Toa mchango kila wakati unapokaribisha wageni

Toa kidogo kila wakati unapokaribisha wageni
kwa kutoa mchango wa asilimia ya malipo yako.
Toa mchango
Mwanamume aliyevaa sweta ya rangi ya chungwa na mwanamke aliyevaa rinda la kijivu wamesimama kwenye mlango wa nyumba wakitabasamu na kuegemeana.

Toa sehemu salama ya kukaa

Tangaza sehemu yako kwa bei iliyopunguzwa kwa watu walio katika nyakati za shida.
Jisajili ili kukaribisha wageni

Kuwa mfadhili

Unaweza kutoa kidogo kila unapokaribisha wageni au kutoa mara moja.

Asilimia 100 inafadhili makazi moja kwa moja

Kiasi chochote unachotoa huenda moja kwa moja kwenye ufadhili wa makazi ya dharura kwa watu wakati wa shida.

Airbnb pia inatoa mchango

Airbnb hushughulikia gharama zote za uendeshaji za Airbnb.org na husamehe ada zote za huduma kwa kila sehemu ya kukaa.

Wageni hukaa bila malipo

Wenyeji hufungua nyumba zao, nyingi kwa punguzo. Michango husaidia kulipia gharama zilizosalia.

Kuwa mwenyeji wa Airbnb.org

Unaweza kutoa makazi ya dharura kwa punguzo.

Washirika wa eneo husika hukagua wageni

Tunafanya kazi na mashirika yasiyotengeneza faida ya eneo husika ili kuwatambua wageni wenye uhitaji mkubwa zaidi.

AirCover na zaidi

Sehemu zote za kukaa zinalindwa na AirCover na wenyeji wanaweza kufikia timu mahususi ya usaidizi.

Pata beji ya mfadhili

Kutoa nyumba yako kunakupa beji ya mfadhili wa Airbnb.org kwenye wasifu wako wa mwenyeji.

Kila sehemu ya kukaa ina simulizi

Kutana na watu walioathiriwa na majanga na wale waliosaidia.