Marianne

Jinsi mama alivyoiweka familia yake salama dhidi ya moto wa mwituni

Familia ya watu watano wamesimama jikoni mwao, wakizungumza na kushikilia vikombe vya kahawa.
Moto wa Daraja Kusini mwa California uliilazimisha familia ya Marianne kuondoka nyumbani kwao.
Marianne na familia yake walipomleta kijibwa kipya kinachoitwa Toby nyumbani kwao huko Wrightwood, California, hawakufikiria kwamba wangeondoka naye siku iliyofuata. Siku ya Jumanne, tarehe 10 Septemba, asubuhi hiyo ilikuwa siku ya kawaida kwao. Binti za Marianne, wenye umri wa miaka 14, 12 na 9, walienda shuleni na alifanyia kazi barazani kwake chini ya anga safi.
Mwanamke aliye kwenye ua wa nyuma anacheza na mbwa wawili, huku watu watatu wakiwa wamesimama kwenye ukumbi upande wa nyuma.
Siku moja kabla ya kuondoka, familia ilikuwa imemleta nyumbani kijibwa kipya kinachoitwa Toby, kifupi cha Toblerone.
Kufikia mapema alasiri, upepo uliongezeka nguvu na majivu yakaanguka kutoka angani kadiri moto ulivyokaribia. Ingawa maafisa walimhakikishia kila mtu mambo yalikuwa sawa, Marianne alichukua hatua na kuwaleta wasichana hao nyumbani kutoka shuleni. Walitazama hali zikizidi kuwa mbaya nje. "Ilikuwa kama taswira ya jehanamu," Marianne alisema. "Mimi na mume wangu tulisema, ‘Wasichana, fungasheni.’" Amri ya kuondoka ikaja haraka baadaye.
"Ilikuwa kama taswira ya jehanamu. Mimi na mume wangu tulisema, ‘Wasichana, fungasheni.’"
—Marianne, mgeni wa Airbnb.org
Mwonekano kutoka nyumbani kwa Marianne unaonyesha anga za rangi ya chungwa iliyokoza kutokana na moto.
Mwonekano kutoka nyumbani kwa Marianne unaonyesha jinsi moto ulivyokaribia. (Picha na Marianne)
Wakati huo huo Airbnb.org ilishirikiana na mashirika yasiyotengeneza faida ya eneo husika katika kaunti ya San Bernardino, Hearts & Lives na Visit Big Bear, ili kuweka watu waliohamishwa kwenye sehemu za kukaa za Airbnb bila malipo. Wenyeji watatu wa Airbnb walijitolea kusaidia washirika kutafuta wageni na kueneza neno kuhusu makazi ya dharura kupitia Airbnb.org. Tara, Katie na Monique walitengeneza fomu za kujisajili, wakazichapisha kwenye mitandao ya kijamii na wakafanya kazi mchana na usiku wakishirikiana na washirika wa eneo husika ili kusaidia kuwapa makazi wahamishwa katika jumuiya zao. “Watu walikuwa wamekata tamaa kabisa,” Tara akasema. "Starehe katika sauti yao waliposikia kwamba wanaweza kupata chumba kwa ajili ya mtoto wao mchanga kutambaa, kufua, kutengeneza mlo, hiyo ni sauti ya shukrani ya kweli." Kwa msaada wa wenyeji na washirika, Airbnb.org iliwakaribisha zaidi ya wakazi 1,000 wa San Bernardino waliohamishwa na moto wa Daraja na Mstari, ikiwemo mamia ya watoto na wanyama vipenzi.
Watu wawili wameketi kwa karibu kwenye kochi katika chumba cha ndani chenye joto, cha mbao, wakionyesha hali ya umoja na utulivu.
Tara na Katie Wenyeji Bingwa wa Airbnb, walisaidia mashirika yasiyotengeneza faida ya eneo husika kuwatambua wageni walio na mahitaji na kuwapa nyumba kwenye Airbnb.

"Starehe katika sauti yao waliposikia kwamba wanaweza kupata chumba kwa ajili ya mtoto wao mchanga kutambaa, kufua, kutengeneza mlo, hiyo ni sauti ya shukrani ya kweli."

—Tara, Mwenyeji Bingwa wa Airbnb huko Big Bear, CA
Picha ya wasifu ya Tara, mwenyeji wa Airbnb.org, iliyo na beji ya alama ya tiki iliyothibitishwa.
Familia ya Marianne, pamoja na Toby, walikuwa miongoni mwa wale waliokaa kwenye sehemu ya Airbnb bila malipo walipokuwa chini ya amri ya kuondoka. "Ulimwengu wetu wote umetuendea mrama. Mwishowe kupata sehemu ambayo tungeweza kupumzika ilikuwa faraja kubwa," alisema. Alikumbuka kufungua vifaa kadhaa vya usafi kwa mara ya kwanza baada ya siku kadhaa. "Lilikuwa jambo dogo sana, lakini lilikuwa na maana kubwa kupata mahali ambapo ningeweza kuweka vitu vyangu na mwishowe kufikiria."
Wasichana wawili wameketi kwenye viti tofauti katika sebule yenye starehe na kuna vifaa vya kuchezea na jiko upande wa nyuma.
Baada ya wiki mbili za kufuatilia moto wa mwituni na kuwa na wasiwasi kuhusu nyumba yao, familia ya Marianne iliweza kurudi nyumbani kwa usalama.
Baada ya wiki mbili wakiwa mbali, familia iliweza kurudi nyumbani salama, ambapo waliungana tena na wanyama wao na wasichana walirudi shuleni. Hii ilikuwa mara ya pili kwa Marianne na mumewe kukimbia moto wa mwituni tangu wahamie Wrightwood mwaka 2015. Huenda isiwe ya mwisho, lakini Marianne alisema anahisi mwenye bahati kuishi katika jumuiya ambapo watu husaidiana sana, hasa wakati wa dharura."Kulikuwa na mambo mengi yasiyojulikana, lakini Airbnb.org ilitoa tumaini na uhakikisho kwamba tungefanikisha hilo, si tu kwa kutumia nguo zilizokuwa tumevaa, bali kwamba tungetunzwa na kupata makao kwa urahisi."

Saidia Airbnb.org

Asilimia 100 ya michango huenda moja kwa moja kwenye ufadhili wa sehemu za kukaa za bila malipo kwa watu wakati wa shida.
Toa mchango