Mwanaolimpiki Mlemavu Vanderson Chaves
Mwanaolimpiki Mlemavu anaendeleza ndoto za Paris 2024 baada ya mafuriko nchini Brazili
Mwezi mmoja kabla ya mchezaji wa mchezo wa kushindana kwa vitara Vanderson Chaves kutarajia kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Paris 2024, mafuriko makubwa yaliharibu nyumba yake huko Rio do Sul, Brazili. Alikuwa mmoja wa watu 600,000 waliohamishwa makwao na maafa hayo.
Kiwango cha maji hatimaye kilifika kwenye dari ya nyumba yake na kubeba vifaa vyake vya mchezo wa kushindana kwa vitara, medali na pasipoti. Vanderson, ambaye alishiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Walemavu jijini Rio de Janeiro mwaka 2016 na Tokyo mwaka 2021, alihofia kwamba mafuriko yanaweza kumzuia kwenda jijini Paris.
Vanderson, ambaye ni mwanatimu wa timu ya Brazili ya mchezo wa kushindana kwa vitara wa viti vya magurudumu tangu mwaka 2013, ni mmoja wa washindani wakuu wa vitara katika mabara ya Amerika Kaskazini na Kusini. Mchezo wa kushindana kwa vitara ulikuja katika maisha yake akiwa katika wakati mgumu. “Haikuwa kupenda mchezo kwa kuuona kwa mara ya kwanza” anasema.
Vanderson alitamani kuwa mchezaji wa soka wa kulipwa. Alipokuwa na umri wa miaka 12, risasi iliyokosa shabaha ilimpiga shingoni na kumlemaza kuanzia kiunoni kwenda chini. “Wazo langu la kwanza lilikuwa, je, nitachezaje soka?” anasema.
Alifanya kazi kwenye Ofisi za Jiji na mchezaji wa mchezo wa kushindana kwa vitara wa viti vya magurudumu ambaye alimhimiza kuujaribu mchezo huo. Vanderson, ambaye hakuwa amewahi kusikia kuhusu mchezo wa kushindana kwa vitara hapo awali, alisema hakupendezwa. Udadisi ulimshinda na mwishowe akaenda kutazama timu ya mwenzake ikifanya mazoezi. Uzoefu huo ulimvutia.
“Kila kitu nilichofikiri nisingeweza kufanya tena, watu hao walifanya.” Vanderson aliamua kufanyia majaribio mchezo wa kushindana kwa vitara na akaupenda mara moja. Tangu wakati huo amesafiri ulimwenguni akishindana katika viwango vya juu zaidi vya mchezo wake. 1 kati ya kurasa 1
Tarehe 4 Mei, 2024, mafuriko yaligharikisha nyumba ya Vanderson. Alikuwa amebakiza mashindano mawili muhimu ili kufuzu kwenda jijini Paris. Mbali na kushinda mfadhaiko wa akili uliotokana na maafa hayo, pia alihitaji vifaa na mahali pa kukaa ili aweze kuendelea na mazoezi.
Wachezaji wa mchezo wa kushindana kwa vitara kutoka nchini Brazili na Marekani walichangia nguo na mavazi ya riadha na Vanderson alipata sehemu ya kukaa ya bila malipo na inayofikika jijini Porto Alegre kupitia Airbnb.org. Akiwa amepata makazi, aliweza kuendelea na mazoezi.
“Kuwa na nyumba kupitia Airbnb.org kumekuwa muhimu kwangu, kwa sababu nina utulivu wa akili na usalama wa kujua kwamba nitamaliza mazoezi yangu. Nitaweza kwenda nyumbani na kupumzika.”

Licha ya vikwazo vingi, Vanderson alisafiri hadi kwenye mchujo na akapata pointi alizohitaji ili kushiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Walemavu. Hajui iwapo au lini ataweza kurejea nyumbani kwake, lakini anatarajia kurudisha medali mpya nchini Brazili.
Tazama Vanderson akishindana kuanzia tarehe 3 Septemba saa 7:00 adhuhuri majira ya CET.

Airbnb.org inawapa makazi waathirika nchini Brazili
Tangu mafuriko yalipotokea, Airbnb.org imetoa sehemu za kukaa za bila malipo kwa wahamishwaji huko Rio do Sul. Kwa ushirikiano na shirika lisilotengeneza faida la Pertence, tumewapa makazi familia zilizo na watoto ambao wana mahitaji maalumu na ulemavu. Pia tumeshirikiana na UNICEF kuwapa makazi waitikiaji wa kwanza wanaosaidia juhudi za misaada ya maafa.
Saidia Airbnb.org
Asilimia 100 ya michango huenda moja kwa moja kwenye ufadhili wa sehemu za kukaa za bila malipo kwa watu wakati wa shida.
Toa mchango