Kufungua nyumba wakati wa janga
Tunashirikiana na jumuiya yetu kutoa makazi wakati wa dharura, kuanzia majanga ya asili hadi migogoro mikubwa.
Tangu mwaka 2012, zaidi ya watu 250,000 wamepata sehemu ya kukaa wakati wa shida
Kupitia jumuiya yetu ya kimataifa ya Wenyeji, wafadhili na mashirika washirika, Airbnb.org iliweza kuwapa watu zaidi ya 140,000 makazi ya muda.
Jinsi Carmen na jumuiya yake walivyoungana baada ya Kimbunga Maria.
Tunazipa jumuiya njia ya kuja pamoja majanga yanapotokea. Kupitia mipango ya Airbnb.org, watu wanaweza kutoa nyumba zao bila malipo kwa majirani ambao wanahitaji kuhamishwa.
Airbnb.org imewasaidia watu 100,000 wanaokimbia vita kupata sehemu za kukaa.
Inaweza kuchukua miaka kwa jumuiya kupona kabisa kutokana na janga kubwa. Airbnb.org husaidia kufadhili sehemu za kukaa kwa wafanyakazi wa misaada ambao wanafanya kazi muhimu ya kujenga upya jumuiya.
Kuunda ulimwengu uliojikita katika kujisikia nyumbani
Airbnb.org inatazamia ulimwengu ambao mtu yeyote anaweza kupata sehemu ya kukaa inayomfanya ahisi amekaribishwa wakati wa mgogoro. Ili kufanikisha maono haya kwa kila mtu, Airbnb.org iliunda ahadi kadhaa kuhusu uanuwai, usawa, ujumuishaji na ufikiaji.