Jinsi tulivyoanza.
Wazo lilitoka kwa mwenyeji
Jiji la New York lilipigwa na Kimbunga Sandy, mojawapo ya vimbunga vibaya zaidi katika historia. Shell, mwenyeji wa Airbnb huko Brooklyn, aliwasiliana na Airbnb na kuomba ikiwa anaweza kutoa eneo lake bila malipo kwa watu ambao walilazimika kuhama. Timu ya Airbnb ilifanya kazi kwa saa nyingi ili kuwezesha nyumba hizo zipatikane haraka kwa wahamiaji na punde wenyeji zaidi ya 1,000 wakafungua nyumba zao kwa wenye uhitaji.
Airbnb inawawezesha wenyeji zaidi kutoa msaada
Airbnb inazindua Chombo cha kushughulikia majanga ambacho kinawaruhusu Wenyeji ulimwenguni kote kutoa nyumba zao bila malipo wakati wa majanga.
Wageni kote ulimwenguni wafungua milango yao kwa wafanyakazi wa misaada
Airbnb inaanza kazi kwa ajili ya tetemeko la ardhi la Nepal na wenyeji wanakaribisha kundi lao la kwanza la wafanyakazi wa misaada na watu wa kujitolea kutoka All Hands and Hearts.
Airbnb inafanya kazi na mashirika yasiyotengeneza faida ili kuelewa jinsi ya kutoa msaada
Ushirikiano huundwa na Wakala wa Shirikisho wa Udhibiti wa Dharura (FEMA) ili kusaidia kusambaza rasilimali za maandalizi ya dharura kwa wenyeji na wageni. Huko Ugiriki na Balkan, Airbnb inaanza kufanya kazi na Mercy Corps na Kamati ya Uokoaji ya Kimataifa kutoa makazi kwa wafanyakazi wa misaada walio katika mstari wa mbele wa janga la wakimbizi wa Siria.
Airbnb pia inaanza kutoa misaada ya makazi kwa mashirika zaidi ya 15 ambayo yanahitaji makazi kwa ajili ya wateja au wafanyakazi wao, ikiwemo Service Year Alliance, Make-a-Wish, na Summer Search.
Jumuiya ya wenyeji yaitikia mifyatuo ya risasi katika kilabu cha usiku cha Pulse
Kwa ombi la serikali ya mtaa, Airbnb, Uber na JetBlue waliungana ili kutoa makazi, ndege na usafiri kwa familia zinazosafiri kwa ndege kwenda mazishi au kuwatembelea wapendwa hospitalini. Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa jumuiya ya wenyeji kujitolea kuwakaribisha watu walioathiriwa na mauaji ya umma kwa kupigwa risasi.
White House yazindua Wito wa Kuchukua Hatua kwa Sekta ya Kibinafsi Kuhusika katika Janga la Wakimbizi Ulimwenguni. Majibu ya Airbnb. Mwanzilishi mwenza wa Airbnb Joe Gebbia alikuwa mmoja wa watendaji 20 walioalikwa na Rais Obama kutoa ahadi kuhusu janga la wakimbizi.
Airbnb inashirikiana na Make-a-Wish wakiwa na lengo la kuipa makao familia moja iliyotoa matamanio kwa siku moja mwaka 2017.
Airbnb inaweka ahadi kwa Kamati ya Uokoaji ya Kimataifa
Kwa kuitikia agizo la rais wa Marekani linalozuia wakimbizi kuingia na kusimamisha kwa muda watu kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi, Airbnb inajizatiti kuwapa makazi wale walioathiriwa na marufuku hayo. Kwa kuitikia, Airbnb pia imeahidi kuchangia USD milioni 4 kwa kipindi cha miaka 4 kwa International Rescue Committee ili kusaidia mahitaji ya makazi ya watu ambao wamehamishwa kwenye makazi yao.
Airbnb inazindua rasmi Open Homes
Katika Siku ya Wakimbizi Ulimwenguni, Airbnb inatangaza kwamba itazidisha juhudi zake za makazi na Open Homes. Mpango huo umewezesha jumuiya ya wenyeji kutoa nyumba zao bila malipo kwa watu walioathiriwa na majanga au kukimbia mizozo.
Jumuiya imesaidia zaidi ya watu 20,000 kufikia sasa
Jumuiya ya Open Homes hushughulikia majanga 4 kwa wakati mmoja. Kimbunga Harvey kinakuwa uamilifu mkubwa zaidi wa jumuiya ya wenyeji. Kwa mwezi mmoja tu, wenyeji wamesaidia zaidi ya watu 2,000 ambao walikuwa wamehamishwa katika majimbo 3. Wakati huo huo, wenyeji walifungua nyumba zao kwa wale walioathiriwa na Kimbunga Irma, Kimbunga Maria, na tetemeko la ardhi la Mexico City.
Airbnb inatangaza mpango wa sehemu za kukaa kwa ajili ya matibabu
Kwenye Mkutano wa Saratani wa Biden, Airbnb inatangaza sehemu za kukaa kwa ajili ya matibabu kwa kushirikiana na Hospitality Homes, Fisher House na Make-A-Wish. Kupitia hiyo, jumuiya ya Open Homes itatoa sehemu za kukaa bila malipo kwa wale wanaosafiri mwendo mrefu kwa ajili ya matibabu.
Wenyeji wanashughulikia majanga mawili tofauti ya moto huko California
Baada ya Moto wa Kambi na Woolsey huko California, zaidi ya wenyeji 2,500 walifungua milango yao na zaidi ya watu 2,300 walipata sehemu ya kukaa.
Airbnb inatengeneza njia kwa ajili ya wenyeji kutoa michango ya kusaidia Open Homes
Wenyeji walitaka njia zaidi za kushiriki katika Open Homes. Kwa kuitikia, Airbnb inatangaza tovuti ya michango ambayo inawaruhusu wenyeji kutoa asilimia ya mapato yao kwa washirika wa Open Homes wasiotengeneza faida ili kusaidia kufadhili sehemu za kukaa kwa wale wanaozihitaji.
Wenyeji wanatoa makazi kwa zaidi ya watu 1,000 walioathiriwa na moto wa msituni wa Australia huko New South Wales na Victoria. Hii inaashiria uamilishaji mkubwa zaidi wa kimataifa wa Open Homes kufikia sasa.
Jumuiya ya wenyeji hupambana na janga la COVID-19
Airbnb inatangaza njia ya wenyeji kutoa makazi kwa wafanyakazi wa huduma ya afya na wahudumu wa dharura kwenye mstari wa mbele wa janga hili.
Airbnb inapanua tovuti yake ya mchango, kwa hivyo mtu yeyote anaweza kutoa mchango kwa mashirika yasiyotengeneza faida ambayo yanasaidia wafanyakazi wa mstari wa mbele kupata sehemu ya kukaa.
Airbnb inatangaza Airbnb.org
Airbnb inaanzisha Airbnb.org na inasherehekea kazi yote ya maana inayofanywa na wenyeji na washirika kupitia Open Homes. Kama shirika lisilotengeneza faida, Airbnb.org itazingatia kuwasaidia watu kushiriki nyumba na nyenzo katika nyakati za matatizo.
Uanuwai, usawa na ujumuishaji ndio muhimu zaidi
Ili kusaidia kuunda ulimwengu unaojikita katika kujisikia nyumbani, Airbnb.org inatangaza hadharani mfululizo wa ahadi ili kuleta matokeo kwa ajili ya uanuwai, usawa na ujumuishaji.
Airbnb.org inatoa ukaribisho mkubwa kwa wakimbizi wa Afghanistani
Airbnb.org imejizatiti kutoa makazi ya muda kwa wakimbizi 20,000 wa Afghanistani kote ulimwenguni. Fedha zinatoka kwa wafadhili wakuu vilevile zinatoka Airbnb. Airbnb.org inashirikiana kwa karibu na mashirika yanayotoa makazi mapya na washirika ili kushughulikia hali inayobadilika kwa haraka.
Airbnb.org inafikia hatua kuu ya kutoa makazi kwa wageni 100,000
Mwaka 2017, timu ambayo baadaye ilikuja kufahamika kama Airbnb.org ilijiwekea lengo la kijasiri la kutoa makazi ya muda mfupi kwa wageni 100,000 wakati wa shida. Kufikia mwezi Desemba mwaka 2021, Airbnb.org imevuka lengo.
Wakimbizi 20,000 kutoka Afghanistani wanapokea makazi ya bila malipo na ya muda
Airbnb.org inawasaidia watu 100,000 wanaokimbia Ukrainia kupata sehemu za kukaa
Airbnb.org inaonesha mwitikio katika majanga ya matetemeko ya ardhi nchini Uturuki na Siria
Airbnb.org inatangaza Mpango mpya wa Ufadhili
Zaidi ya watu 1,800 walioathiriwa na moto wa Maui wanapata sehemu za kukaa za dharura
Kutana na bodi yetu.
Jennifer Bond
Jay Carney
Joe Gebbia
Sharyanne McSwain
Catherine Powell
Rich Serino
Jocelyn Wyatt
Jinsi tunavyofanya kazi.
Kushirikiana na mashirika yasiyotengeneza faida
Airbnb.org inatoa misaada kwa mashirika yasiyotengeneza faida ambayo huwaunganisha watu na makazi ya muda, rasilimali na msaada maalumu wakati wa majanga. Pia tunatoa ufikiaji wa makazi bila malipo na yenye punguzo yanayotolewa na jumuiya ya wenyeji wa Airbnb.
Kuwekeza katika usawa
Tunaamini kutumia nguvu na rasilimali zetu ili kuchangia ulimwengu ulio na haki zaidi. Airbnb.org inawekeza katika mashirika yenye mikakati na mipango ambayo inaambatana na dhamira yetu ya kuendeleza usawa katika jumuiya.
Kuelewa matokeo ya mipango yetu
Tunakusudia kuweka ramani ya matokeo ya mpango wetu wa ufadhili na makazi ili kuboresha ustawi wa kisaikolojia, kupunguza mzigo wa kifedha na kuimarisha jumuiya na hisi ya wageni kujisikia nyumbani.
Ushirikiano na ruzuku
Airbnb.org haikubali maombi ya ufadhili wa fedha kwa wakati huu. Tutashiriki taarifa kuhusu mzunguko wetu unaokaribia wa ruzuku na mashirika yasiyotengeneza faida yanayostahiki moja kwa moja.
Jinsi tunavyofanya kazi na Airbnb, Inc.
Airbnb.org ni shirika huru lisilotengeneza faida la 501(c)(3) linaloungwa mkono na umma. Airbnb.org hutumia teknolojia, huduma na rasilimali nyinginezo za Airbnb, Inc bila malipo ili kutekeleza lengo la misaada la Airbnb.org. Airbnb.org ni chombo tofauti na huru kutoka Airbnb, Inc. Airbnb, Inc haitozi ada ya huduma kwa sehemu za kukaa za Airbnb.org kwenye tovuti yake.
Mpango wa Open Homes uliundwa na Airbnb na ulichochewa na ukarimu wa wenyeji wa Airbnb, kama njia ya kuwasaidia watu wanaohitaji kupata makazi ya muda. Mpango wa Open Homes kwa sasa unabadilishwa kuwa Airbnb.org na Airbnb.org itaendeleza juhudi za mpango huo, kulingana na lengo la misaada na mwito wa Airbnb.org.