Wape watu mahali pa kuishi wakati wa shida.

Karibisha wageni kwenye sehemu ya kukaa.

Katika hali ya dharura, unaweza kujitokeza kuisaidia jumuiya yako kwa kutoa sehemu ya kukaa kwa watu walio katika shida, ikiwemo wakimbizi.
Anza kukaribisha wageni
Nani utasaidia
Sehemu yako inaweza kutoa starehe kwa familia inayohama kwa sababu ya moto wa msitu, mkimbizi anayesafiri kwa ajili ya kuokoa maisha au mfanyakazi wa msaada aliyehamia eneo lililoathiriwa na kimbunga kwa ajili ya kutoa msaada.
  • "Tulijua wafanyakazi wanaotoa huduma muhimu walikabili hatari katika maeneo yao ya ajira. Tulikuwa na wazo, tunaweza kuwasaidia vipi kwa kiwango kikubwa?”

    Erika, Mwenyeji wa Airbnb.org kwa ajili ya wahudumu wa dharura walio kwenye mstari wa mbele

Safari ya sehemu ya kukaa

Jinsi ya kuanza kukaribisha wageni

Uko tayari kujisajili? Tutakuelekeza ili kukuonyesha jinsi ya kuunda tangazo lako na kulishiriki na wageni. Ili kuanza, utahitaji tu sehemu nzuri na usiku mchache unaopatikana.

Ustahiki na utambulisho wa mgeni hukaguliwa

Kwa baadhi ya sehemu za kukaa, Airbnb.org huthibitisha utambulisho na ustahiki wa mgeni. Kwa sehemu nyingine za kukaa, Airbnb.org hushirikiana na baadhi ya mashirika ili kuthibitisha utambulisho wa wageni pamoja na hitaji lao la makazi ya muda. Mara nyingi, utaweza kupiga gumzo na wawakilishi wa mpango au wageni watarajiwa wakati wa mchakato wa kuweka nafasi.

Tuko hapa kwa ajili yako

Airbnb inawapa Wenyeji na wageni AirCover. AirCover kwa ajili ya Wenyeji inajumuisha bima ya dhima ya USD milioni 1, ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 3 na kadhalika. Vikomo na vighairi fulani hutumika.

Toa mchango ili kufadhili sehemu za kukaa.

Mamilioni ya watu ulimwenguni kote wamehamishwa kutoka kwenye nyumba zao kwa sababu ya mgogoro na maafa. Michango husaidia kulipia gharama za malazi ya muda.
Toa mchango sasa
Asilimia 100 ya mchango wako huwasaidia watu walio kwenye shida.
Tunasamehe ada zote za huduma, kwa hivyo mchango wako wote unawasaidia watu kupata sehemu ya kukaa wakati wanaihitaji zaidi. Mchango wako unaweza kusaidia familia ya wakimbizi kupata sehemu ya kukaa wanapowasili kwa mara ya kwanza au mfanyakazi wa msaada kupumzika baada ya siku yenye shughuli nyingi.
  • "Nilikuja nchini hapa kama mkimbizi na nitajitahidi kadiri niwezavyo kutoa msaada kama nilivyopewa msaada."

    Aime, mfadhili huko Davie, Florida, Marekani

    "Nimejihusisha na maendeleo ya jumuiya, huduma na uenezi kwa miaka thelathini na mitano. Ninaamini kuwasaidia wengine kwa njia halisi, endelevu na zenye kujenga."

    Michael, mfadhili huko Philadelphia, Pennsylvania, Marekani

Jinsi mchango wako unavyokwenda zaidi ya matarajio

Airbnb pia inatoa mchango

Tunayo timu ya wataalamu wasiotengeneza faida na wa teknolojia ambao wanajitahidi ili kuzidisha matokeo yetu. Airbnb hushughulikia gharama zote za uendeshaji ili kuwezesha jambo hilo.

Ada zote za uchakataji zinasamehewa

Hatuchukui kiasi chochote cha fedha, kwa hivyo mchango wako wote unawasaidia watu kupata makazi wanapoyahitaji zaidi.

Michango inakatwa kodi

Mchango wako unatozwa kodi kwa kiwango kinachoruhusiwa chini ya sheria za eneo husika. Utapokea risiti ya kodi ili kukusaidia kufuatilia ukataji wako.

Maswali yako yajibiwa

Kutana na wenyeji na wageni wetu.

Hebu tuwasiliane.