Mlipuko wa bomba la gesi nchini Malesia

Amirul aliwasaidia majirani zake kurejea hali ya kawaida baada ya maafa

Amirul na mkewe Izzati wameketi kwenye kochi wakitabasamu wakiangalia kamera

Amirul alikuwa akisherehekea siku ya pili ya Idi na familia yake nyumbani kwao huko Putra Heights, Malesia, asubuhi ya tarehe 1 Aprili, 2025, waliposikia sauti kubwa ya injini. Waliangalia dirishani na kuona kile kilichoonekana kama mpira wa moto. Jengo lilikuwa likitetemeka. Bila muda wa kufikiri au kuchukua kitu chochote, walimchukua binti yao na kukimbia nje ya mlango, mbali na hatari.Mlipuko wa bomba la gesi lililokuwa karibu ulisababisha moto uliowakosesha zaidi ya watu 500 makazi, kujeruhi watu 150 na kuharibu nyumba 81.

Miguu ya mtoto imefungwa kwa bendeji

Amirul na jamaa zake walipata majeraha ya kuungua ya kiwango cha pili na cha tatu kutokana na moto huo.

Amirul aliishi huko Putra Heights pamoja na mke wake na familia yake. Wakati wa mlipuko huo, Amirul alikuwa pamoja na mke wake, wazazi wake na jamaa zake tisa. Wote walitoroka lakini walipata majeraha ya kuungua ya kiwango cha pili na cha tatu. Walipoteza nyumba yao na familia ilisambaa kati ya hospitali na makazi ya jumuiya. Amirul alisikia kuhusu makazi ya dharura ya bila malipo kupitia Airbnb.org na akaweka nafasi ya ukaaji wa muda wa mwezi mmoja huku yeye na familia yake wakisubiri suluhisho la muda mrefu kutoka kwa serikali ya eneo husika. Makazi yao yalikuwa karibu na hospitali, ambapo Amirul na jamaa zake walisafiri kwenda na kurudi kwa ajili ya matibabu ya majeraha ya kuungua.

“Nyumba ni mahali salama. Mahali ambapo tunajisikia vizuri. Tunaweza kuwa hapo, bila wasiwasi wowote.”

Familia ya Amirul imekusanyika kwenye meza ya chakula cha jioni huku chakula kikiwa juu ya meza

Amirul ni Mwenyeji Bingwa na alikuwa mwepesi kuweka nafasi ya makazi yake ya dharura, lakini majirani zake wengi ambao pia walikuwa kwenye makazi hawakuifahamu tovuti hiyo. Ingawa alikuwa kwenye kiti cha magurudumu kwa sababu ya majeraha ya kuungua kwenye miguu yake, Amirul alienda kwenye mikutano ya jumuiya ya eneo husika ili kuwaambia majirani zake kuhusu Airbnb.org na kuwasaidia wajisajili ili kupokea makazi ya dharura ya bila malipo.

Amirul, mwenyeji aliye kwenye kiti cha magurudumu, anazungumza na Matin kutoka Airbnb.

"Kama mwenyeji, nilihisi kwamba nilikuwa na jukumu la kujitokeza na kuongoza jumuiya kupitia mchakato huo."

Baada ya ukaaji wa Amirul wa Airbnb.org, yeye na familia yake walihamia fleti nyingine katika jengo hilohilo. Alirudi kazini na familia yake inaendelea kupona. Wanapanga kujenga upya huko Putra Heights.

Jihusishe

Jiunge na jumuiya ya kimataifa inayotoa makazi ya dharura wakati wa shida.

Pata maelezo zaidi

Kila sehemu ya kukaa ina simulizi

Kutana na watu walioathiriwa na majanga na wale waliosaidia.