Familia ya Benn yashikamana baada ya mioto ya mwituni

Familia ya Benn ni sehemu ya Altadena, California, ambapo wanajulikana kama familia ya muziki. Watoto saba wa Laurie na Oscar walikua wakiimba katika shule ya eneo hilo, kanisani na kwenye hafla za jumuiya na wanaendelea kuimba nyimbo pamoja hadi leo.
Familia ya Benn wameishi huko Altadena tangu miaka ya 1950 na walikuwa mojawapo ya familia za kwanza za Watu Weusi kununua nyumba katika eneo hilo. Watoto walilelewa umbali mfupi kutoka kwa bibi yao na shangazi na wajomba zao. Walichuma matunda kutoka kwenye ua wao wa nyuma.
"Tulikuwa na bahati ya ajabu kulelewa katika jumuiya kama hiyo, iliyo na familia zilizo kama zetu ambazo ziliweza kupata thamani katika umiliki wa nyumba na kwamba vizazi vilikuwa sehemu yake," alisema Loren Benn, mwenye umri mkubwa zaidi kati ya watoto wa Laurie na Oscar.
“Kupoteza nyumba ni jambo moja. Kuhisi kama umepoteza urithi kidogo ni jambo jingine.”
Wakati moto wa Eaton ulipoenea huko Altadena, uliteketeza nyumba ya mzazi wa Loren, nyumba ya bibi yake na nyumba ya kaka yake. “Kupoteza nyumba ni jambo moja. Kuhisi kama umepoteza urithi kidogo ni jambo jingine,” Loren alisema.

Familia ya Benn walipoteza nyumba ambapo walilelea watoto saba na makazi mengine kadhaa katika kitongoji hicho.
Familia ya Benn walipohamishwa, walidhani watarudi baada ya siku chache. Oscar alikuwa akitumia oksijeni na walikuwa waangalifu zaidi ili kuepuka moshi huo. Ikawa wazi kwamba hawaendi nyumbani na Loren alituma ombi la makazi ya dharura kupitia Airbnb.org na 211 LA. Wanafamilia kumi na moja wa Benn, ikiwemo wajukuu watatu wa Oscar na Laurie, walikaa bila malipo kwenye Airbnb kwa zaidi ya mwezi mmoja huku wakifikiria cha kufanya baadaye.

Kukaa pamoja kulikuwa muhimu kwa familia ya Benn, ambao wamezoea kuishi pamoja na kusaidiana katika maisha yao ya kila siku. "Tulipofika hapa, ilitupa hali ya kawaida," alisema Laurie. Usiku mmoja waliandaa tambi. Ilikuwa mara yao ya kwanza kula chakula kilichopikwa nyumbani tangu walipopoteza nyumba zao. Mjukuu mdogo zaidi alitembea kwa mara ya kwanza kwenye nyumba hiyo.
"Tunajua kwamba haitakuwa sawa, lakini matumaini yetu ni kwamba jumuiya itabaki jinsi ilivyo na kupitia hali hii pamoja nasi."

Wakati wa ukaaji wao wa Airbnb.org, familia ya Benn walipata makazi ya muda mrefu kwa mwaka uliofuata. Wanapanga kurudi Altadena na kujenga upya si nyumba zao tu, bali mtindo wa maisha ambao wameujua sikuzote.
Jihusishe
Jiunge na jumuiya ya kimataifa inayotoa makazi ya dharura wakati wa shida.
Pata maelezo zaidiKila sehemu ya kukaa ina simulizi
Kutana na watu walioathiriwa na majanga na wale waliosaidia.