Msaada wa mioto ya mwituni ya Los Angeles
Tumewapa makazi zaidi ya watu 22,000 walioathiriwa na mioto ya mwituni na tunaendelea kutoa usaidizi.
Msaada wa mioto ya mwituni ya Los Angeles
Tumewapa makazi zaidi ya watu 22,000 walioathiriwa na mioto ya mwituni na tunaendelea kutoa usaidizi.

Mioto ya mwituni iliyoanza tarehe 7 Januari, 2025 jijini Los Angeles iliwahamisha makwao zaidi ya watu 200,000 na watu 29 walipoteza maisha yao. Mioto hiyo iliharibu majengo zaidi ya 12,000 na kusababisha uharibifu kwa vitongoji vizima.
Usaidizi endelevu


Toa sehemu ya kukaa
Tangaza sehemu yako kwa bei iliyopunguzwa kwa watu wakati wa shida.
Matokeo yetu
Mara tu baada ya mioto ya mwituni kuanza, Airbnb.org ilishirikiana na shirika lisilotengeneza faida 211 LA ili kutoa makazi ya dharura bila malipo kwa watu walioathiriwa. Tulimpa mgeni wetu wa kwanza makazi ndani ya saa 24 na tumetoa makazi ya dharura kwa zaidi ya watu 22,000.
Takwimu za ramani kutoka tarehe 9 Januari hadi tarehe 2 Machi, 2025
Watu walitaka kukaa karibu na nyumbani na kuweka nafasi ya Airbnb karibu na makazi yao ya msingi, hivyo kuwaruhusu kuwaweka watoto shuleni, kubaki karibu na kazini na kuendelea kushirikiana na jumuiya ya mahali walipo.
22,000
Wageni waliokaribishwa
2,300
Wanyama vipenzi waliokaribishwa
1,000
Wahudumu wa dharura waliokaribishwa
Simulizi za wenyeji na wageni
Kadiri wanavyoanza kurejelea hali ya kawaida, wanajumuiya wanaendelea kusaidiana.
Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Je, ninawezaje kupata sehemu ya kukaa ya dharura ya Airbnb.org?
Nani anaweza kuweka nafasi ya sehemu kupitia Airbnb.org?
Watu ambao wameathiriwa na mioto ya mwituni huko Los Angeles wanaweza kustahiki kuweka nafasi ya sehemu ya kukaa ya dharura kupitia Airbnb.org, ambayo inajumuisha watu waliohamishwa makwao na wafanyakazi wa msaada wanaosaidia katika wadhifa rasmi. Airbnb.org inafanya kazi na mashirika ya serikali na washirika wasiotengeneza faida ili kusaidia kuamua ustahiki. Pata maelezo zaidi
Je, ninaweza kutoa nyumba yangu kwa bei kamili kwenye Airbnb kwa ajili ya wageni na pia kuitoa bila malipo au kwa punguzo wakati wa dharura kupitia Airbnb.org?
Ndiyo. Una kalenda moja, hivyo wageni hawataweza kuweka nafasi mara mbili kwenye sehemu yako.
Nitajuaje kwamba nafasi iliyowekwa imetoka kwenye Airbnb.org?
Wenyeji wanaarifiwa wakati wa mchakato wa kuweka nafasi wakati ombi la kuweka nafasi ni la sehemu ya kukaa ya dharura kupitia Airbnb.org.
Ni nini hutokea wakati ukaaji wa mgeni unamalizika?
Wageni wa Airbnb.org wana wajibu wa kutoka wakati uliokubaliwa kulingana na rekodi ya nafasi iliyowekwa. Ikiwa mgeni atashindwa kutoka kwa wakati, Airbnb ina timu mahususi ya wahudumu maalumu wa usaidizi ambao watashirikiana na mgeni ili kuwezesha kutoka.
Mimi si mwenyeji wa Airbnb, lakini nataka kutoa nyumba yangu kufuatia maafa ya asili. Nifanye nini?
Unaweza kujisajili ili kukaribisha wageni kupitia Airbnb.org pekee, kumaanisha kwamba utakaribisha wageni wanaohitaji sehemu za kukaa za dharura pekee na utatoa sehemu yako bila malipo. Sehemu yako haitapatikana kwa wageni kuweka nafasi ya sehemu za kukaa zisizo za dharura.
Pata maelezo zaidi kuhusu majibu yetu
Kutana na watu walioathiriwa na majanga na wale waliosaidia.