Msaada kwa walioathiriwa na Kimbunga Melissa
Saidia kutoa makazi ya dharura bila malipo kwa watu walioathiriwa na Kimbunga Melissa.
Toa mchangoMsaada kwa walioathiriwa na Kimbunga Melissa
Saidia kutoa makazi ya dharura bila malipo kwa watu walioathiriwa na Kimbunga Melissa.
Toa mchango
Jinsi tunavyoitikia
Ili kuwasaidia wale walioathiriwa na Kimbunga Melissa, Airbnb.org inashirikiana na mashirika yakiwemo All Hands & Hearts, Church World Service, Haiti Air Ambulance, International Organization for Migration (IOM), Project HOPE na Team Rubicon, miongoni mwa mengine, ili kutoa makazi kwa ajili ya timu zao za wahudumu wa dharura katika eneo lote la Karibea.Nchini Jamaika, Airbnb.org inafanya kazi moja kwa moja na IOM na maafisa wa serikali ili kutoa makazi ya dharura bila malipo kwa ajili ya wafanyakazi muhimu na watu waliohamishwa na dhoruba.
Jinsi ya kusaidia

Toa mchango
Asilimia 100 ya mchango wako itafadhili makazi ya dharura kwa watu walioathiriwa na Kimbunga Melissa na maafa mengine.
Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Ninawezaje kupata sehemu ya kukaa ya dharura ya Airbnb.org?
Kwa sasa, Airbnb.org haikubali maombi ya moja kwa moja kwa watu wanaotafuta usaidizi wa dharura. Badala yake, Airbnb.org itashirikiana na mashirika ya serikali na washirika wasiotengeneza faida wa eneo husika ili kupata watu wanaohitaji sehemu za kukaa za dharura. Pata maelezo zaidi
Ni nani anayestahiki kuweka nafasi ya sehemu ya kukaa kupitia Airbnb.org?
Watu ambao wameathiriwa na Kimbunga Melissa wanaweza kustahiki kuweka nafasi ya sehemu ya kukaa ya dharura kupitia Airbnb.org, ambayo inajumuisha watu waliohamishwa na wafanyakazi wa msaada wanaosaidia katika nyadhifa rasmi. Airbnb.org inafanya kazi na mashirika ya serikali na washirika wasiotengeneza faida ili kusaidia kuamua ustahiki. Pata maelezo zaidi
Je, ninaweza kutoa nyumba yangu kwa bei kamili kwenye Airbnb kwa ajili ya wageni na pia kuitoa bila malipo au kwa punguzo wakati wa dharura kupitia Airbnb.org?
Ndiyo. Una kalenda moja, hivyo wageni hawataweza kuweka nafasi mara mbili kwenye sehemu yako.
Nitajuaje kwamba nafasi iliyowekwa imetoka kwenye Airbnb.org?
Wenyeji wanaarifiwa wakati wa mchakato wa kuweka nafasi wakati ombi la kuweka nafasi ni la sehemu ya kukaa ya dharura kupitia Airbnb.org.
Ni nini hutokea wakati ukaaji wa mgeni unamalizika?
Wageni wa Airbnb.org wana wajibu wa kutoka wakati uliokubaliwa kulingana na rekodi ya nafasi iliyowekwa. Ikiwa mgeni atashindwa kutoka kwa wakati, Airbnb ina timu mahususi ya wahudumu maalumu wa usaidizi ambao watashirikiana na mgeni ili kuwezesha kutoka.
Mimi si mwenyeji wa Airbnb, lakini nataka kutoa nyumba yangu kufuatia maafa ya asili. Nifanye nini?
Unaweza kujisajili ili kukaribisha wageni kupitia Airbnb.org pekee, kumaanisha kwamba utakaribisha wageni wanaohitaji sehemu za kukaa za dharura pekee na utatoa sehemu yako bila malipo. Sehemu yako haitapatikana kwa wageni kuweka nafasi ya sehemu za kukaa zisizo za dharura.
Je, mchango wangu unamsaidia nani?
Mchango wako kwa Airbnb.org unalipia makazi ya dharura kwa familia na wahudumu wa dharura ambao wanahitaji sehemu ya kukaa kwa sababu ya Kimbunga Melissa au maafa mengine.Asilimia 100 ya mchango wako huenda kufadhili makazi ya dharura bila malipo kwa watu walioathiriwa, si kwa gharama za uendeshaji. Gharama za uendeshaji za Airbnb.org zinagharimiwa na Airbnb. Airbnb.org inafanya kazi kwa kujitegemea kama shirika lake lenyewe lisilotengeneza faida la 501(c)(3).
Pata maelezo zaidi kuhusu miitikio yetu
Kutana na watu walioathiriwa na maafa na wale waliosaidia.




