Saidia kuwapa makazi wakimbizi 100,000 wanaokimbia kutoka nchini Ukrainia
Toa sehemu za kukaa bila malipo au kwa punguzo kupitia Airbnb.org au uchangie ili kusaidia fedha zetu zitimize mengi zaidi.
Usaidizi wako huleta tofauti
Airbnb.org inafadhili makazi ya muda mfupi kwa hadi watu 100,000 wanaokimbia Ukrainia. Tunawasaidia wageni wetu wakimbizi bila kujali utaifa, mbari, kabila au jinsi wanavyojitambulisha.
Unaweza kutoa msaada kwa kutoa sehemu za kukaa za muda bila malipo au kwa punguzo kupitia Airbnb.org au kutoa mchango ili kufadhili sehemu za kukaa.
Toa sehemu ya kukaa
Anza kukaribisha wageni bila malipo au kwa punguzo.
Namna kukaribisha wageni kunavyofanya kazi
- Utatoa kitanda cha starehe na vistawishi vya msingi kwa ajili ya mahali popote kuanzia siku kadhaa hadi wiki kadhaa. Pata maelezo zaidi kuhusu kukaribisha wageni wakimbizi
- Airbnb.org inashirikiana na mashirika yasiyotengeneza faida ambayo huwakagua wageni wakimbizi ili kuona kama wanastahiki na kuwasaidia kabla ya ukaaji wao, wakati wa ukaaji wao na baada ya hapo.
- Airbnb inawapa Wenyeji AirCover: bima ya dhima ya USD milioni 1, ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 3 na kadhalika, bila gharama kwa Wenyeji. Vikomo na vighairi fulani hutumika.
Toa mchango
Kila mchango husaidia kutimiza uhitaji muhimu wa sehemu za kukaa za dharura kwa wale wanaokimbia nchi ya Ukrainia na wengine walio katika shida.
Jinsi kutoa mchango kunavyofanya kazi
- Asilimia 100 ya mchango wako utatumiwa kuwawezesha watu kupata makazi ya muda mfupi.
- Sehemu za kukaa hazina malipo kabisa kwa wageni walio kwenye mpango wetu.
- Michango inatozwa kodi kwa kiwango kinachoruhusiwa chini ya sheria za kodi za eneo lako.
Je, unahitaji usaidizi?
Hatutoi makazi moja kwa moja kwa watu binafsi kwa wakati huu. Airbnb.org hushirikiana na washirika wengine wasiotengeneza faidia ambao huweka nafasi na kuratibu sehemu za kukaa kwa ajili ya wageni wakimbizi.
Kile ambacho washirika wetu wasiotengeneza faida hufanya
Washirika wetu ni mashirika yasiyotengeneza faida ambayo husaidia kuwakaribisha wakimbizi. Mashirika haya yanasaidia wateja wao kupata makazi na kadhalika. Mapendekezo kutoka kwa mashirika yasiyotengeneza faida yanakubaliwa kwa mwaliko tu.
Kile ambacho Airbnb.org inafanya
Airbnb.org hutoa ruzuku na teknolojia kwa washirika wetu wasiotengeneza faida, ambao huratibu makazi ya muda kwa ajili ya wateja wao.
Jinsi Airbnb inavyotoa michango
Kuwasaidia Wenyeji
Airbnb inawapa Wenyeji AirCover: bima ya dhima ya USD milioni 1, ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 3 na kadhalika, bila gharama kwa Wenyeji. Vikomo na vighairi fulani hutumika.
Kufadhili sehemu za kukaa
Airbnb na wafadhili wanachangia fedha kwa ajili ya sehemu za kukaa za muda kwa hadi wakimbizi 100,000 wanaokimbia Ukrainia.
Kusamehe ada
Airbnb inasamehe ada za Wenyeji na wageni kwenye sehemu zote za kukaa za Airbnb.org kwa ajili ya wakimbizi.