Mafuriko katika Ziwa Naivasha

Airbnb.org inashirikiana na Forum for Women in Development, Democracy and Justice ili kutoa makazi ya dharura bila malipo kwa wahudumu wa dharura wanaosaidia jumuiya zilizoathiriwa na mafuriko ya hivi karibuni katika Ziwa Naivasha, Kenya.

Jinsi ya kusaidia

Ikiwa ungependa kusaidia kutoa sehemu za kukaa bila malipo kwa watu walioathiriwa na mafuriko katika Ziwa Naivasha, unaweza kutoa mchango kwa Airbnb.org. Asilimia 100 ya michango huenda moja kwa moja kwa makazi ya dharura. Ikiwa wewe ni mwenyeji wa Airbnb, unaweza kujisajili ili kutoa ukaaji wenye punguzo kwa wakazi walioathiriwa. Airbnb hutoa ada zake za huduma za mwenyeji kwa Airbnb.org kwa ajili ya sehemu hizi za kukaa na huwapa wenyeji AirCover kwa kila nafasi inayowekwa.

Una maswali?

Tafadhali wasiliana nasi kupitia contact@airbnb.org