Kuweka familia na wanyama vipenzi wao pamoja
Kwa sababu ya Jinx, Airbnb.org inaweza kutoa makazi zaidi ya dharura bila malipo kwa watu na wanyama vipenzi wao baada ya maafa.

Kutana na Maile, Kai na mbwa wao
"Airbnb.org isingekuwepo, kiukweli, tungekuwa tunahama hama nyumba hivi sasa na tungekuwa tunalala kwenye gari letu," Maile alisema kuhusu sehemu yake ya kukaa ya muda mfupi ya bila malipo kupitia Airbnb.org. “Nilifurahi kufua nguo. Nilifurahi kuwaogesha mbwa. Nilifurahi kupika mlo kamili. Nilikuwa nikipika kifungua kinywa, chakula cha mchana na chakula cha jioni. Hivyo ndivyo ninavyofanya kwa kawaida na nilijisikia vizuri.”
Soma simulizi yaoKutomwacha nyuma mnyama kipenzi yeyote wakati wa maafa
Wakati wa kuhamishwa wakati wa maafa, asilimia 32 ya watu walimwacha nyuma mbwa mmoja, kulingana na ASPCA ya Marekani.Airbnb.org huwasaidia watu waliohamishwa makazi kuweka nafasi ya malazi yanayowafaa wanyama vipenzi ili familia nzima iweze kukaa pamoja.

Jinx inatoa mchango ili kufadhili sehemu za kukaa za dharura zinazowafaa wanyama vipenzi
Kupitia usaidizi wa Jinx, Airbnb.org inaweza kuwapa watu wengi zaidi na wanyama vipenzi wao mahali pazuri pa kupata nafuu pamoja.Mchango wa Jinx kwa Airbnb.org unaweza kufadhili zaidi ya usiku 900 wa makazi ya dharura bila malipo kwa familia zilizohamishwa na maafa.

Shukrani kwa washirika wetu katika

Jinx ni chapa ya kisasa ya chakula cha wanyama vipenzi inayozingatia ustawi wa wanyama vipenzi, yaani mbwa na paka.
Pata maelezo zaidi