Mlipuko wa bomba la gesi nchini Malesia
Majirani wakiwasaidia majirani

Jayden aliposikia kuhusu bomba la gesi ambalo lililipuka huko Putra Heights mwezi Aprili mwaka 2025, mara moja aliwasiliana na mtandao wake ili kusaidia watu ambao walikuwa wamehamishwa makwao na maafa hayo.
Kama Mkurugenzi Mtendaji wa HostPlatform, Jayden anafanya kazi na maelfu ya wenyeji kote nchini Malesia na Kusini-Mashariki mwa Asia ili kuwasaidia kusimamia matangazo yao. Kwa hivyo, alipogundua kuwa Airbnb.org ilikuwa ikitoa makazi ya dharura ya wiki mbili bila malipo kwa watu walioathiriwa na mlipuko, yeye na wenzake, Ken na Eunice, waliwahimiza wenyeji huko Putra Heights kufanya nyumba zao zipatikane kwa wale walio na uhitaji.
“Tunajivunia kuweza kusaidia na kuiauni jumuiya kwa sababu hili ni jukumu letu kama Wamalesia”
Kujizatiti kwao kulienea zaidi ya kutoa msaada, walihudhuria pia mikutano ya jumuiya kwenye makao ambapo manusura wengi walikuwa wakikaa, wakiwasaidia kujisajili kupitia Airbnb.org
Jihusishe
Jiunge na jumuiya ya kimataifa inayotoa makazi ya dharura wakati wa shida.
Pata maelezo zaidiKila sehemu ya kukaa ina simulizi
Kutana na watu walioathiriwa na majanga na wale waliosaidia.
1 kati ya kurasa 1