Katikati mwa Texas

Kupata kimbilio baada ya mafuriko

The Hill Country flood memorial wall in Kerrville, Texas

“Saa 11 asubuhi, tuliamshwa na liwali mmoja akigonga mlango wetu. Alituambia nyumba chache mtaani zilisombwa kabisa na mafuriko.”

- Skylyn, mgeni wa Airbnb.org

Asubuhi na mapema tarehe 5 Julai, 2025, Skylyn, mwenzi wake na mtoto wake mwenye umri wa miezi 10 waliamka na kuona maji yakiingia nyumbani kwao. Mvua ilikuwa ikinyesha usiku uliotangulia na sasa ua wao wa mbele ulikuwa mto unaotiririka. Mafuriko yaliyovunja rekodi yalisomba nyumba nzimanzima Katikati mwa Texas ikiwemo za majirani zao.

Baada ya mafuriko katikati mwa Texas, unaweza kuona uharibifu wa miti.

Mara moja, Skylyn alijaribu kuhama pamoja na familia yake, lakini lori lake lilikuwa limekwama kwenye matope na maji zaidi ya futi tatu. Skylyn alipata habari kwamba Airbnb.org ilikuwa ikitoa makazi ya dharura bila malipo kwa wale walioathiriwa na mafuriko kupitia All Hands and Hearts. Aliwasiliana na akaweza haraka kuweka nafasi ya sehemu ya kukaa ya Airbnb.org iliyo karibu. Sehemu hii ilimpa mwanawe sehemu ya kucheza na kumruhusu kufikiria hatua zinazofuata.

Skylyn, mgeni wa Airbnb.org, amemshika mtoto wake mwenye umri wa miezi 10 kwenye kiti katika Airbnb walikohamia kutoka kwenye mafuriko.

Skylyn na mwanawe, Waylon

“Ilinipa faraja kubwa kuona mwanangu akijifurahisha wakati huo wa mfadhaiko.”

- Skylyn, mgeni wa Airbnb.org

Wahudumu wa dharura, wafanyakazi wa kujitolea na timu za dharura walihamasishwa haraka ili kuwasaidia wale walioathiriwa Katikati mwa Texas. Timu hizi bado zinawasaidia wakazi kupata nafuu na kujiandaa kujenga upya kwa kuondoa matope, vifusi na nyenzo zilizojaa maji kutoka kwenye nyumba zilizoharibiwa na mafuriko.

Kikundi cha wafanyakazi wa kujitolea kutoka All Hands and Hearts wanapika jikoni kwenye sehemu yao ya kukaa ya Airbnb.org.

"Ni vigumu sana kuelewa jinsi maji yenye kimo cha futi 30 yanavyoonekana, halafu unazungumzia ukuta wa maji wenye kimo cha futi 30 unaotiririka mtoni."

- Alix, mgeni na mfanyakazi wa kujitolea wa Airbnb.org
Ukuta wa kumbukumbu ya mafuriko ya Hill Country jijini Kerrville, Texas

Wafanyakazi wengi wa kujitolea wamekuwa wakifanya kazi saa 20 kwa siku, kwa hivyo kukaa karibu kumekuwa muhimu. Airbnb.org imeweza kutoa makazi kwa vikundi vya kujitolea vya hadi watu 12 ili kuhakikisha kuwa wanaweza kupumzika, kushiriki milo na kupata nguvu tena pamoja.Airbnb.org imetoa makazi ya dharura bila malipo Katikati mwa Texas kwa zaidi ya wageni 350.

Jihusishe

Jiunge na jumuiya ya kimataifa ya watu wanaotoa makazi ya dharura wakati wa shida.

Pata maelezo zaidi

Kila sehemu ya kukaa ina simulizi

Kutana na watu walioathiriwa na maafa na wale waliosaidia.