Desemba 2022

Kuunda ulimwengu uliojikita katika kujisikia nyumbani

Mchoro na Helen Li

Dhamira ya Airbnb.org ni kufungua uwezo wa kushiriki sehemu, nyenzo na usaidizi wakati wa uhitaji. Lakini si kila mtu aliye na ufikiaji sawa wa nyenzo hizi. Ndiyo sababu tumejizatiti kuhakikisha uanuwai, usawa, ujumuishaji na ufikiaji ambao ni muhimu katika kazi yetu ya kila siku.

Ahadi zetu za msingi za DEIA

Mwezi Aprili mwaka 2021, Airbnb.org ilitangaza ahadi tatu za msingi za kuwa na uanuwai, usawa na ujumuishaji. Ahadi hizi zinaunda uhusiano wetu na wageni na Wenyeji; ushirikiano wetu na mashirika yasiyotengeneza faida na mashirika ya serikali na timu yetu ya Airbnb.org.

Kama shirika, tumeahidi:

  1. Elekeza mpango na kazi yetu kwa watu kutoka jumuiya zilizotengwa ambao kihistoria wamepata ufikiaji mdogo wa rasilimali kutokana na ukandamizaji wa kijamii, kitamaduni, kiuchumi na kisiasa.
  2. Jitahidi kuhakikisha kwamba mgeni yeyote anayekuja kupitia Airbnb.org anapata ubora sawa wa huduma na ukaaji.
  3. Unda timu anuwai na jumuishi, ambayo inajumuisha, kama hatua ya kuanzia, kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka 2025 angalau asilimia 33 ya wafanyakazi wetu wa Marekani watakuwa wa jumuiya za watu wachache wenye uwakilishi mdogo.

Mwaka 2022, tuliona hitaji la kujumuisha ufikiaji kama sehemu ya kipekee ya ahadi yetu; tutasasisha ahadi yetu ya kuutimiza mwaka 2023.

Hivi ndivyo tunavyotekeleza ahadi yetu

Ili kutimiza ahadi zetu za sasa za DEIA:

  • Kufanya kazi na mashirika ya jumuiya na yasiyotengeneza faida ambayo yanashiriki ahadi yetu ya kuwa na usawa. Migogoro inapotokea, timu zetu hujitahidi kufanya kazi na mashirika ya mahali husika yanayohudumia jumuiya zilizotengwa. Hivi karibuni tulishirikiana na mashirika kama vile:
    • Each One Teach One, ambalo linasaidia watu wenye ulemavu na raia wasiotoka Ukrainia waliohamishwa makwao na mgogoro nchini Ukrainia
    • Black Women for Black Lives, ambalo lilitoa sehemu za kukaa bila malipo nje ya nchi kwa wanafunzi 2,000 wa Kiafrika walioko nchini Ukrainia
    • Oram, kampuni tanzu ya Alight, ambayo ilisaidia watu wa LGBTQ+ waliokimbia Ukrainia kupata makazi na usaidizi wa kijamii jijini Berlin na miji mingine ya Ulaya
  • Kushirikiana na wataalamu wanaoongoza wa uanuwai na usawa ili kutusaidia kutathmini na kuboresha kazi yetu kuhusu ahadi hizi. Shirika tunaloshirikiana nalo kimsingi limekuwa We All Count, ambalo linakuza mtazamo unaolenga usawa wa utafiti. Mwaka 2022, waliisaidia Airbnb.org kutekeleza utafiti wa majaribio ili kuelewa vyema matukio yanayowakabili watu ambao wamepata makazi ya muda wakati wa shida kupitia Airbnb.org. Kupitia mchango huu, tunaunda njia yetu ya kufuatilia maendeleo yetu na kuhakikisha kwamba tunatimiza ahadi yetu.
  • Kujumuisha mbinu za ubunifu za usawa kwenye kazi zetu. Usimulizi wetu wa visa kuhusu kiwewe na kanuni za ubunifu zinazozingatia usawa hutuongoza katika kutunga simulizi kuhusu kazi tunayofanya na wageni, Wenyeji na washirika wetu. Tunashirikiana katika kufanya maamuzi kwa ubunifu, kuheshimu machaguo ya lugha za watu na jinsi wanavyochagua kuwakilishwa kupitia picha.
  • Kuhakikisha kwamba ahadi yetu ya usawa inawafikia wafanyakazi. Lengo letu, ifikapo mwishoni mwa mwaka 2025, ni angalau asilimia 33 ya wafanyakazi wetu wa Marekani wawe wa jumuiya za watu wachache wenye uwakilishi mdogo. Tunafafanua jumuiya za watu wachache wenye uwakilishi mdogo nchini Marekani kama wale wanaojitambulisha na mbari/kabila moja au zaidi kati ya yafuatayo: Mhindi Mmarekani au Mzaliwa wa Alaska; Mweusi au Mmarekani Mwafrika; Mhispania au Mlatino; Mzaliwa wa Hawaii au Mzaliwa wa Kisiwa Kingine cha Pasifiki.

    Tulipoweka ahadi hii awali, jumuiya za watu wachache wenye uwakilishi mdogo walikuwa asilimia 19 ya wafanyakazi wetu wa wakati wote. Kufikia tarehe 30 Septemba, 2022, jumuiya za watu wachache wenye uwakilishi mdogo ni asilimia 28 ya wafanyakazi wa Airbnb.org wa wakati wote. Tunajua kwamba inahitaji kazi ya mara kwa mara ya kushiriki, kudumisha na kuinua vipaji mbalimbali ili kuendelea kufaidika na mitazamo mbalimbali na tutaendelea kuweka kipaumbele kwa usawa katika kuajiri na kudumisha.

Tumejizatiti kufikiria njia mpya za kuzingatia usawa katika kazi yetu, kuleta matokeo katika jumuiya ambazo zimekumbwa na mgogoro na kusaidia kuunda ulimwengu uliojikita katika kujisikia nyumbani na uponyaji.

Mchoro na Helen Li