Tetemeko la Ardhi nchini Indonesia
Tarehe 18 Agosti, matetemeko matatu ya ardhi yalitokea nchini Indonesia ndani ya saa 24. Tetemeko la ardhi lenye nguvu zaidi lilikuwa na ukubwa wa 7.7 na lilikumba pwani ya Flores. Tetemeko hilo lilifuatiwa na mitetemeko zaidi ya 230 ya ardhi na onyo la tsunami.Airbnb.org inashirikiana na Caritas Indonesia ili kutoa makazi ya dharura bila malipo kwa wahudumu wa dharura na watu wenye uhitaji.
Ikiwa ungependa kusaidia kutoa sehemu za kukaa bila malipo kwa watu walioathiriwa na tetemeko la ardhi, unaweza kutoa mchango kwenye Airbnb.org. Asilimia 100 ya michango huenda moja kwa moja kwenye makazi ya dharura. Ikiwa wewe ni mwenyeji wa Airbnb, unaweza kujisajili ili kutoa ukaaji wenye punguzo kwa wakazi walioathiriwa. Airbnb hutoa ada zake za huduma za mwenyeji kwa Airbnb.org kwa ajili ya sehemu hizi za kukaa na huwapa wenyeji AirCover kwa kila nafasi inayowekwa.