Michezo ya Olimpiki na Olimpiki ya Walemavu ya Paris 2024
Sherehekea Timu za Olimpiki na Olimpiki ya Walemavu za Wakimbizi
Timu za Olimpiki na Olimpiki ya Walemavu za Wakimbizi za Paris 2024 zimeundwa na wanariadha 46 ambao wanawakilisha zaidi ya watu milioni 120 waliohamishwa makwao kote ulimwenguni. Wakfu wa Wakimbizi wa Olimpiki na Airbnb.org wameshirikiana kusherehekea timu na kuongeza uelewa wa idadi inayoongezeka ya watu wanaolazimika kukimbia nyumba zao.

Wasaidie wakimbizi ulimwenguni kote
Wakfu wa Wakimbizi wa Olimpiki na Airbnb.org zinashiriki ahadi ya kutoa usaidizi kwa watu waliohamishwa makwao. ORF imetoa ufikiaji wa michezo salama kwa zaidi ya vijana 400,000 waliohamishwa makwao. Airbnb.org imetoa makazi ya bila malipo, ya muda kwa zaidi ya wakimbizi na watafuta hifadhi 210,000.
Tunaamini kwamba kila mtu anastahili sehemu ya kujisikia nyumbani. Jiunge nasi kuwasaidia watu waliohamishwa makwao kwenye Michezo ya Olimpiki na Olimpiki ya Walemavu ya Paris 2024 na ulimwenguni kote.Matokeo yetu
Tangu mwaka 2020, Airbnb.org imefungua uwezo wa kushiriki sehemu, rasilimali na usaidizi wakati wa shida.
220,000 na zaidi
Wageni waliokaribishwa
Milioni 1.4
Sehemu za kukaa za dharura, bila malipo
134
Nchi zilizo na wenyeji wa Airbnb.org
Jihusishe
Toa mchango
Asilimia 100 ya michango huenda moja kwa moja kwenye ufadhili wa sehemu za kukaa za bila malipo kwa watu wakati wa shida.
Jisajili ili kukaribisha wageni
Katika hali ya dharura, unaweza kujitokeza kwa ajili ya jumuiya yako kwa kutoa sehemu ya kukaa.