Wasaidie watu walioathiriwa na Kimbunga Helene
Airbnb.org inatoa makazi ya dharura ya bure kwa manusura wa Kimbunga Helene, watu wa kujitolea na wahudumu wa dharura.
Dhamira ya Airbnb.org ni kufungua uwezo wa kushiriki sehemu, nyenzo na usaidizi wakati wa uhitaji.
Kutana na jumuiya yetu
Vita vya wenyewe kwa wenyewe viliharibu kila kitu walichokuwa wamejenga. Sasa wanaanza tena maisha yao mbali na nyumbani kwa msaada wa jumuiya yao mpya.
Kupitia jumuiya yetu ya kimataifa ya Wenyeji, wafadhili na mashirika washirika, Airbnb.org iliweza kuwapa watu zaidi ya 140,000 makazi ya muda.
Jinsi Carmen na jumuiya yake walivyoungana baada ya Kimbunga Maria.
Airbnb.org imewasaidia zaidi ya watu 135,000 wanaokimbia vita kupata sehemu za kukaa.
Inaweza kuchukua miaka kwa jumuiya kupona kabisa kutokana na janga kubwa. Airbnb.org husaidia kufadhili sehemu za kukaa kwa wafanyakazi wa misaada ambao wanafanya kazi muhimu ya kujenga upya jumuiya.
Kuunda ulimwengu uliojikita katika kujisikia nyumbani
Airbnb.org inatazamia ulimwengu ambao mtu yeyote anaweza kupata sehemu ya kukaa inayomfanya ahisi amekaribishwa wakati wa mgogoro. Ili kufanikisha maono haya kwa kila mtu, Airbnb.org iliunda ahadi kadhaa kuhusu uanuwai, usawa, ujumuishaji na ufikiaji.