Kufungua nyumba wakati wa janga
Tunashirikiana na jumuiya yetu kutoa makazi wakati wa dharura, kuanzia majanga ya asili hadi COVID-19.
Watu 100,000 wamepata eneo la kukaa wakati wa shida tangu mwaka 2012.
Jinsi Carmen na jumuiya yake walivyoungana baada ya Kimbunga Maria.
Tunazipa jumuiya njia ya kuja pamoja majanga yanapotokea. Kupitia mipango ya Airbnb.org, watu wanaweza kutoa nyumba zao bila malipo kwa majirani ambao wanahitaji kuhamishwa.
Wakimbizi na wanaotafuta hifadhi wanakabiliwa na changamoto nyingi wanapohamia nchi mpya. Kuwa na makazi ya bila malipo na ya muda mfupi huwasaidia kuwa na utulivu wa akili wanapoanza maisha yao mapya.
Jifunze jinsi tunavyofanya kazi na washirika kama CORE ili kusaidia upatikanaji wa chanjo kwa usawa.
Inaweza kuchukua miaka kwa jumuiya kupona kabisa kutokana na janga kubwa. Airbnb.org husaidia kufadhili sehemu za kukaa kwa wafanyakazi wa misaada ambao wanafanya kazi muhimu ya kujenga upya jumuiya.
Kuunda ulimwengu uliojikita katika kujisikia nyumbani: ahadi za Airbnb.org
Leo, kutokana na miaka 8 ya mafunzo na uzoefu, tunatangaza mfululizo wa ahadi za kuwa na uanuwai, usawa na ujumuishaji.
Tunasaidia mashirika mengine yasiyotengeneza faida kuleta matokeo ya kudumu.
