Kufungua nyumba wakati wa janga

Tunashirikiana na jumuiya yetu kutoa makazi wakati wa dharura, kuanzia majanga ya asili hadi COVID-19.

Watu 75,000 wamepata eneo la kukaa wakati wa shida tangu mwaka 2012.

Kote ulimwenguni, wenyeji wa Airbnb hutoa usaidizi wakati unahitajika zaidi. Kutana na watu ambao hufanya iwezekane.

Tunasaidia mashirika mengine yasiyotengeneza faida kuleta matokeo ya kudumu.

Kutana na washirika wachache waliosaidia kuunda Airbnb.org.

International Medical Corps

IMC hutoa huduma za dharura za matibabu na nyinginezo zinazohusiana na wale walioathiriwa na majanga ulimwenguni na huwapatia watu mafunzo wanayohitaji ili kuacha kutegemea misaada na kuanza kujitegemea.

International Rescue Committee

IRC hukabiliana na majanga mabaya zaidi ya kibinadamu ulimwenguni na huwasaidia watu ambao maisha na riziki yao imeharibiwa na mizozo na maafa ili waweze kuishi, kurudia hali yao ya kawaida na kupata udhibiti wa maisha yao ya baadaye.

HIAS

HIAS ni shirika lisilotengeneza faida la Kiyahudi ulimwenguni ambalo hutoa ulinzi na msaada kwa wakimbizi, wanaotafuta hifadhi na watu wengine waliohamishwa kwa nguvu ulimwenguni kote.

Build Change

Build Change ni shirika la kuzuia na kukabiliana na majanga linalounda suluhisho za makazi bora pamoja na jumuiya za eneo husika.

Community Organized Relief Effort

CORE inaongoza katika maandalizi, kukabiliana na majanga na juhudi za uokoaji kwa jamii zilizoathiriwa na au zilizo katika hatari ya mgogoro.

Shirikisho la Kimataifa la Chama cha Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu

IFRC ndiyo mtandao mkubwa zaidi wa ufadhili wa kibinadamu ulimwenguni, unaojumuisha Mashirika 192 ya Vyama vya Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu yanayofanya kazi kuokoa maisha na kukuza hadhi kote ulimwenguni.
Nembo ya Airbnb.org
Nembo ya Mercy Corps

Pamoja, tunaweza kujenga upya.

Mnamo Agosti 2018, matetemeko ya ardhi yaligonga kisiwa cha Lombok nchini Indonesia. Wafanyakazi wa misaada kutoka Mercy Corps walipelekwa kufanya kazi ya kurejesha hali ya kawaida katika eneo hilo na wakapata jumuiya na mahali pazuri pa kukaa.